Ongeza wateja mmoja mmoja
- Fungua Contacts kwenye menyu kisha bonyeza Add contacts.
- Andika namba ya simu. Jina, barua pepe na siku ya kuzaliwa ni hiari, lakini ukiweka jina unaweza kuandika ujumbe wa kibinafsi.
- Hifadhi. Mteja huyo anaonekana kwenye orodha yako.
Leta faili zima
- Andaa faili la CSV au Excel lenye column inayoitwa
phone. Column hizi ni hiari:name,emailnadate_of_birth(iandikwe YYYY-MM-DD, kwa mfano 1990-04-27). - Kwenye ukurasa wa Contacts bonyeza Import CSV / Excel kisha chagua faili lako.
Tumia orodha
- Bonyeza Create list kutengeneza orodha kama “Wazazi wa Darasa la 1” au “Wateja maalum (VIP)”, kisha tumia Manage members au Add contacts to list kuijaza.
- Wateja ambao hawako kwenye orodha yoyote wanaonekana chini ya Uncategorized.
- Kwenye ukurasa wa Send, chagua All contacts, orodha moja, au chagua watu mmoja mmoja.
Kitu kikienda vibaya
| Tatizo | Cha kufanya |
|---|---|
| Baadhi ya mistari haikuingia | Mistari hiyo haikuwa na namba sahihi ya simu. Rekebisha namba kwenye faili lako kisha uingize tena. |
{name} inaonekana tupu kwenye ujumbe wangu | Mteja huyo hana jina lililohifadhiwa. Ongeza jina, au andika ujumbe bila {name}. |
Miongozo inayohusiana
Unahitaji msaada?
Timu yetu inajibu siku za kazi, Jumatatu hadi Jumamosi, kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 12 jioni (8:00 hadi 18:00, saa za Afrika Mashariki).
Skrini zinaweza kuonekana tofauti kidogo kwenye simu yako au baada ya sisi kuziboresha. Hatua zinabaki zilezile.