Ruka hadi mwongozo
BulkSMS
English

Settings, timu na usalama

Linda akaunti yako, sasisha taarifa za biashara yako na uwaalike wafanyakazi wenzako.

Miongozo yote

Taarifa zako na nenosiri

  • Fungua Settings kusasisha taarifa za biashara yako: aina ya biashara, mkoa na wilaya.
  • Tumia Change password mara kwa mara. Chagua nenosiri ambalo hulitumii mahali pengine popote.
  • Washa Two-factor authentication kwa usalama zaidi. Baada ya nenosiri lako, tunakuuliza pia namba ya uthibitisho.

Mwalike timu yako

  1. Fungua Team. Chagua kualika By phone au By email kisha weka taarifa za mfanyakazi mwenzako.
  2. Chagua nafasi (role) yake kisha tuma mwaliko. Ana siku 7 za kukubali.
  3. Mwaliko haukufika? Tumia Resend invitation, au mtumie kiungo cha mwaliko kinachoonekana kwenye ukurasa. Unaweza pia Remove member kwenye ukurasa huohuo.

Audit log inaonyesha nani alifanya nini kwenye akaunti. Inasaidia pale watu kadhaa wanapotuma ujumbe.

Arifa

Washa arifa kwenye Settings ili tukufikishie taarifa kwenye browser yako. Kwenye app ya simu, arifa zako ziko chini ya More.

Funga akaunti yako

Unaweza kufuta akaunti yako kupitia Settings, au kupitia More kwenye app ya simu. Credit ambazo hujazitumia zinapotea ukifuta, kwa hiyo zitumie kwanza. Ukifuta kwa makosa, wasiliana nasi ndani ya siku 30. Maelezo yako kwenye ukurasa wa kufuta akaunti.

Fungua Settings

Unahitaji msaada?

Timu yetu inajibu siku za kazi, Jumatatu hadi Jumamosi, kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 12 jioni (8:00 hadi 18:00, saa za Afrika Mashariki).

Skrini zinaweza kuonekana tofauti kidogo kwenye simu yako au baada ya sisi kuziboresha. Hatua zinabaki zilezile.