Pakua na uingie
- Fungua ukurasa wa kupakua kisha chagua Android au iPhone. App ni bure. Inahitaji Android 8.0 au mpya zaidi, au iOS 15.1 au mpya zaidi.
- Fungua app kisha ingia kwa namba ileile ya simu na nenosiri unalotumia kwenye tovuti.
- Unaweza pia kufungua akaunti mpya ndani ya app.
Unachoweza kufanya
- Tuma SMS kwa namba moja, kikundi au orodha yako yote, na upange ujumbe utumwe baadaye.
- Ongeza salio kwa pesa za simu na uone salio lako kwenye skrini ya mwanzo.
- Hifadhi wateja, leta namba kutoka kwenye simu yako, omba jina la mtumaji (Sender ID) na tuma KYC.
- Soma arifa zetu chini ya More, na fungua Help & Support kuwasiliana nasi.
- Badilisha lugha ya app kati ya Kiingereza na Kiswahili kwenye Settings.
Akaunti yako ni ileile kila mahali. Unachofanya kwenye tovuti kinaonekana kwenye app, na kinyume chake.
Miongozo inayohusiana
Unahitaji msaada?
Timu yetu inajibu siku za kazi, Jumatatu hadi Jumamosi, kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 12 jioni (8:00 hadi 18:00, saa za Afrika Mashariki).
Skrini zinaweza kuonekana tofauti kidogo kwenye simu yako au baada ya sisi kuziboresha. Hatua zinabaki zilezile.